Wanawake 3 Waliokutwa na Bangi Wahukumiwa Miaka 30 Jela – Video
2026-02-05 - 13:48
Mahakama ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mhe. Kimaro, imewahukumu kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja washtakiwa watatu baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi. Mshtakiwa wa kwanza, Debora Mwita Marwa, alikutwa na hatia ya kusafirisha mirungi yenye uzito wa kilogramu 25.5. Mshtakiwa wa pili ni Jackline Chacha Mwita, naye alitiwa hatiani kwa kusafirisha mirungi yenye uzito wa kilogramu 13.3. Katika shtaka lingine, mshtakiwa wa tatu, Debora Mwita Marwa, alikutwa na hatia ya kusafirisha mirungi bunda 24. Mahakama ilieleza kuwa makosa hayo ni kinyume na Kifungu cha 16(1)(2)(a) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Sura ya 95, Marejeo ya Mwaka 2023. Washtakiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti na maafisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.