Vyakula Ambavyo Husaidia Kupunguza Presha Ya Kupanda
2026-02-24 - 03:36
Presha ya kupanda inaweza kupelekea athari kubwa na mbaya sana kwenye afya ya mtu. Presha ya kupanda isipotibiwa ama mtu asipofuata masharti ya kuishi na ugonjwa huu madhara makubwa yanaweza kutokea. Kifo, kupasuka kwa mishipa ya damu, kupalalaizi, kuharibika kwa figo na moyo kushindwa kufanya kazi na kupata shambulio la moyo yote haya yanaweza kuwa ni matokeo ya presha ya kupanda pindi isipotibiwa ama mtu asipofata masharti.:- Unaweza kupambana na presha kwa kufuata mashari kama kufanya mazoezi, kula vyakula salama kwa presha, kupunguza misongo ya mawazo, kupunguza kula chumvi, kupunguza uzito, kupunguza ama kuacha sigara na pombe. Miongoni mwa vyakula salama kwa presha ni kama 1.Mboga za majani ambazo zina madini ya potassium kwa wingi. Madini haya ni mujarabu sana katika kulinda na kuimarisha afya ya moyo. Ulaji wa mboga hizi unaweza kuwa ni njia ya kujilinda na presha ya kupanda. Miongoni mwa mboga hizi ni kama spinachi 2.Maziwa: maziwa ni katika vyakula vyenye madini ya calcium kwa wingi na pia yana mafuta kwa uchache. Hali zote mbili hizi ni muhimu kwa afya ya moyo. 3.Ndizi; ndizi ni katika matunda yenye madini ya potassium kwa wingi. Ulaji wa ndizi unaweza kuwa ni msaada mzuri kwa kulinda mwili dhidi ya presha ya kupamda. 4.Mayai 5.Samaki aina ya salmon na wanaofanana nao. 6.Ulaji wa mbegu za mimea kama maboga na alizeti 7.Kitunduu thaumu: unaweza kutumia vitunguu thaumu kwa kula ama kutafuna, ni vyema kufunga mdomo wakati unapotafuna. 8.Makomamanga; unaweza kula atunda hili kama juisi ama kula kawaida. HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPANDWA NA PRESHA 1.Muweke mgonjwa kwenye sehemu tulivu na iliyopowa 2.Mpunguzie nguo na abakiwe na ngue nyepesi na chache 3.Unaweza kumpepea ana muweke kwenye feni 4.Mpe vitunguu saumu atafune, na afunge mdomo wakati anatafuna 5.Kama hali itaendelea mpeleke kituo cha afya kilicho karibu. Stori na Elvan Stambuli, Global Digital