TheTanzaniaTime

Vikundi Vya Mawasiliano Vya Majeshi ya SADC Vyajengewa Uwezo

2026-03-03 - 06:37

Vikundi vya Mawasiliano vya Majeshi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) vimekutana kujenga uwezo na kuimarisha uelewa wa pamoja katika fani ya mawasiliano. Mkutano huo umefanyika leo, Machi 2, 2025, katika Hoteli ya Madinat Al Bahr, Unguja, Zanzibar. Akifungua mkutano kwa niaba ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali Amri Salim Mwami amesema mawasiliano bora yanahitaji vifaa vya kisasa na mafunzo endelevu ili kuongeza weledi na ufanisi katika utendaji. Aidha, Brigedia Jenerali Meshack Mosime kutoka Botswana amesema mkutano huo umekuwa na manufaa makubwa kwa nchi wanachama na washiriki binafsi, hasa katika kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu. Mkutano huo umehudhuriwa na wawakilishi wa majeshi kutoka nchi wanachama wa SADC.

Share this post: