TheTanzaniaTime

Video: Waziri Mkuu Amtumbua Muuguzi Aliyemfanyia Upasuaji Mjamzito Nyumbani

2026-03-04 - 14:28

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa muuguzi wa Mkoa wa Tabora anayeshutumiwa kumfanyia mgonjwa upasuaji nyumbani kwake, kwenye kochi, kinyume na sheria na taratibu za utoaji huduma za afya. Akizungumza na wananchi jijini Dodoma, Dkt. Nchemba ameeleza kusikitishwa na tukio hilo, akibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuboresha sekta ya afya, ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya na ajira kwa wahudumu. Aidha, Waziri Mkuu ameagiza Jeshi la Polisi kumkamata muuguzi huyo kwa hatua za kisheria, huku mamlaka husika za usajili na utoaji leseni za uuguzi zikielekezwa kumfutia leseni mara moja.

Share this post: