Video: Serikali Yaidhinisha Rasmi Marekebisho ya Katiba ya Simba
2026-02-18 - 13:07
Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imeidhinisha rasmi marekebisho ya Katiba ya klabu ya Simba baada ya kukamilika kwa mchakato wa kisheria uliokuwa chini ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Michezo. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Februari 18, 2026, Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Abel Ngilangwa, amesema marekebisho hayo yamefanyika kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zote zinazosimamia vyama vya michezo nchini. “Napenda kuufahamisha umma kuwa mchakato wa uchambuzi, tathmini na uidhinishaji wa marekebisho ya Katiba ya Klabu ya Simba umekamilika kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa Sura ya 49 na kanuni zake,” – amesema Ngilungwa
Share this post: