TheTanzaniaTime

Video: Rais Samia – ”Wakinikera Mimi Nabwatuka Tu”

2026-02-09 - 10:18

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Februari 09, 2026, amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam. Viongozi walioapishwa ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Makatibu Tawala wa Mikoa, Naibu Makatibu Wakuu, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango pamoja na Mabalozi. Katika hotuba yake baada ya uapisho huo, Rais Samia amewapa viongozi hao maelekezo mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu yao, akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji, uadilifu na kufanya kazi kwa maslahi ya wananchi. Aidha, Rais Samia ametumia nafasi hiyo kueleza sababu za uamuzi na misimamo yake, akijibu kauli za baadhi ya watu wanaomsema vibaya, huku akisisitiza kuwa maamuzi anayoyafanya yanalenga kulinda maslahi mapana ya Taifa na kuimarisha utendaji wa Serikali.

Share this post: