TheTanzaniaTime

Video: Polisi Wanawatafuta Wanawake Waliompiga Mwenzao Kwa Mwiko

2026-02-09 - 15:40

Jeshi la Polisi limetangaza kuanza uchunguzi kuhusiana na picha mjongeo (video) inayosambazwa kupitia mitandao ya kijamii, ikiwaonyesha wanawake wawili wakimpiga mwanamke mmoja kwa kutumia mwiko, huku wakimshambulia kwa maneno. Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, tukio hilo linadaiwa kuchochewa na madai kwamba mwanamke aliyeshambuliwa alimdhalilisha mmoja wa wanawake hao kupitia mtandao wa Facebook, akimtuhumu kuiba waume za watu. Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi wote wanaowafahamu wanawake wanaoonekana katika video hiyo kutoa taarifa kwa vyombo vya dola kwa njia yoyote iliyo rahisi kwao, ili kusaidia kuwafikia na kuwakamata kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi yao. Jeshi hilo limekemea vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na kusisitiza kuwa migogoro yote inapaswa kushughulikiwa kwa kufuata taratibu za kisheria.

Share this post: