TheTanzaniaTime

Video: Msanii Janka Rino Afariki Dunia Kwa Kifua Kikuu

2026-02-27 - 07:58

Aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva na mwanzilishi wa kundi la LWP Majitu, pamoja na kuwa sehemu ya kundi la Maingizo lililoundwa na mastaa kama Bishanga, Waridi Rich Rich na wengine, Janka Rino amefariki dunia usiku wa jana. Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na mdogo wake, ambaye amesema Janka alifariki katika Hospitali ya Temeke alikokuwa amelazwa. Inadaiwa kuwa msanii huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kifua kwa muda mrefu hadi umauti ulipomkuta. Kwa sasa msiba upo nyumbani kwao Temeke Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo saa saba mchana katika Makaburi ya Chang’ombe.

Share this post: