Video: Makaburi Yanafukuliwa, Nyumba Zinajengwa, Wananchi Walia
2026-02-07 - 15:19
Ni kutoka Kimani mtaa wa Kinyamwezi kata ya Pugu ambapo kuna mgogoro kati ya wananchi pamoja na wananchi ambao wanadai Bi Elizabeth Simon yupo katika eneo hilo kinyuma na taratibu, ambapo eneo hilo ni eneo maalumu ambalo wameelekezwa na serikali ya mtaa kuwa ni eneo ya maziko. Aidha wananchi hao wanadai Mama huyo amefukua makaburi hayo na kwenda kutupa mabaki ya miili ya wapendwa wao. Kwa upande wa Mtuhumiwa huyo amezungumza na GlobalTV na kufafanua kilichotokea na kukana kufukua makaburi hayo na pia ameonesha nyaraka za mahakamani za kushinda kesi hiyo ambapo mahakama ilimpa maelekezo ya nini cha kufanya.
Share this post: