TheTanzaniaTime

Video: Majambazi 9 Wakiri Kumuua Bodaboda Tabora, RC Chacha Aeleza

2026-02-18 - 10:27

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, ameeleza kuwa jumla ya watu tisa wanaodaiwa kuwa majambazi wamekamatwa kufuatia oparesheni maalum iliyofanyika mkoani humo baada ya tukio la mauaji ya dereva bodaboda. Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara, Chacha amesema watuhumiwa hao walikamatwa kupitia msako uliohusisha vyombo vya ulinzi na usalama, na kwamba baada ya mahojiano ya awali wamekiri kuhusika na tukio hilo. Amesisitiza kuwa uongozi wa mkoa hautavumilia vitendo vya uhalifu vinavyohatarisha maisha ya wananchi, akibainisha kuwa yuko tayari kuchukua hatua kali zaidi kuhakikisha wahusika wote wanatiwa nguvuni. Ameongeza kuwa oparesheni hiyo itaendelea hadi pale vyombo vya dola vitakapojiridhisha kuwa mtandao wote wa wahalifu umevunjwa, huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku bila hofu yoyote.

Share this post: