Video: Iran Yafyatua Msururu wa Makombora Kuwait, Uwanja wa Ndege Washambuliwa
2026-03-28 - 12:54
Msururu wa mashambulizi ya drones na makombora wapiga mataifa ya Ghuba; uwanja wa ndege wa Kuwait na kambi ya Marekani yashambuliwa. Hali ya usalama katika ukanda wa Mashariki ya Kati imezidi kuwa tete kufuatia msururu wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (drones) na makombora ya balistiki yaliyolenga miundombinu muhimu nchini Kuwait, Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia. Mashambulizi hayo, yanayohusishwa na Iran pamoja na washirika wake, yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali na kujeruhi wanajeshi pamoja na raia.
Share this post: