Tuzo za Wabunifu nchini Zilivyonoga Usiku wa Kuamkia Leo Mlimani City
2026-02-13 - 01:10
Pichani ni matukio mbalimbali jinsi tuzo za Wabufu zilizofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar zilivyonoga. Miongoni mwa tuzo zilizotolewa ni tuzo ya runinga bora ya mtandaoni (Best Online Media 2025) ambapo Global Tv iliibuka kidedea na kuacha bonge la shangwe ukumbini hapo. Angalia baadhi ya matukio; Msanii wa vichekesho JK Comedian (kulia) akimsalimia kwa madaha Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group na Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mh. Eric Shigongo kwenye hafla hiyo. Muigizaji wa Tamthiliya ya Kombelela maarufu kwa jina la Binti Msumi akimtaja mmoja wa washindi. Dada wa Bilionea na Mfadhili wa Simba SC, Mohames Dewj aitwae Fatema Dewj akiwa kwenye pozi na tuzo aliyotunukiwa. Mwandishi mkongwe wa Global TV, Imelda Mtema naye akifuatilia kinachoendelea kwenye hafla hiyo. Mwanmitindo maarufu hapa nchini, Mustapha Hassanali akielekea jukwaani kuchukua tuzo yake. Staa wa Muvi za Kibongo, Kajala Masanja akishuka jukwaani baada ya kumkabidhi mshindi tuzo. HABARI / PICHA NA RICHARD BUKOS GPL