TheTanzaniaTime

Trump Afuta Video ya Sokwe ya Obama, Asema Hataomba Msamaha – Video

2026-02-07 - 08:08

Rais wa Marekani, Donald Trump, amefuta video yenye kipande cha ubaguzi wa rangi alichochapisha kwenye mitandao ya kijamii kilichomlinganisha Rais wa zamani Barack Obama na Mkewe Michelle Obama na sokwe. Hata hivyo, kwa mujibu wa NBC News Trump amesema hataomba msamaha kwa kuchapisha video hiyo. Video hiyo, yenye muda wa rakribani dakika moja, ilihusu madai ya udanganyifu kwenye uchaguzi wa mwaka 2020, lakini mwishoni ilionyesha sura za familia hiyo ya Obama zilizopachikwa juu ya vichwa vya sokwe huku wimbo wa “The Lion Sleeps Tonight” ukipigwa. Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa usiku, Trump alisema: “Bila shaka nakataa sehemu za ubaguzi wa rangi za video hii, lakini sina mpango wa kuomba msamaha.” Awali, Ikulu ya Marekani ilijitetea kwa kusema video hiyo ilitoka kwenye video ya vichekesho vya mtandaoni ‘meme’ vya mtandaoni, lakini baada ya kupokelewa kwa hasira kutoka kwa waaharakati na baadhi ya wanasiasa wakiwemo wa chama chake, video hiyo ilifutwa. Msemaji wa Ikulu alisema: “Mfanyakazi mmoja wa Ikulu kwa bahati mbaya alichapisha video hiyo. Tayari imefutwa.” Trump hakujibu moja kwa moja Ijumaa usiku kuhusu ni mfanyakazi gani alichapisha video hiyo au kama atafutwa kazi.

Share this post: