TheTanzaniaTime

Tishio la Vita kati ya Marekani na Iran Lazidi Kuongezeka Baada ya Onyo la Trump

2026-01-28 - 16:05

Meli ya kijeshi ya Marekani inayoongozwa na USS Abraham Lincoln ni kubwa zaidi kuliko ile iliyotumwa Venezuela kabla ya kuondolewa kwa Nicolás Maduro. Hatari ya kuzuka kwa vita kati ya Marekani na Iran inaonekana kuongezeka, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuonya kuwa muda unakwisha kwa Iran kukubali makubaliano, huku akidai kuwa meli Armada kubwa ya kijeshi ya Marekani inasogea kwa kasi kuelekea nchini humo. Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Rais Trump amesema meli hiyo ya kivita, inayoongozwa na manowari ya kubeba ndege USS Abraham Lincoln, ni kubwa zaidi kuliko ile iliyotumwa Venezuela kabla ya kuondolewa kwa Nicolás Maduro mapema mwezi huu, na kwamba ipo tayari kutekeleza majukumu yake “kwa kasi na nguvu kubwa endapo itahitajika”. Trump amesema: “Tunatumaini Iran itakuja haraka mezani na kujadiliana makubaliano ya haki na usawa hakuna silaha za nyuklia makubaliano yatakayokuwa mazuri kwa pande zote. Muda umekwisha, jambo hili ni la dharura.” “Kama nilivyowaambia Iran hapo awali, FANYENI MAKUBALIANO. Hawakufanya hivyo, ndipo kulikuwa na ‘Operesheni Midnight Hammer’ iliyosababisha uharibifu mkubwa Iran. Shambulio lijalo litakuwa baya zaidi. Msiruhusu hilo litokee tena.”Alisema. Rais wa Marekani Donald Trump akiongea na wanahabari. Kauli hizo ndizo onyo kali zaidi hadi sasa zikionyesha kuwa Trump anaweza kuamuru shambulio la kijeshi la haraka endapo Iran itakataa kujadiliana kuhusu mustakabali wa mpango wake wa nyuklia. Wanadiplomasia wa Ulaya wamesema walikuwa wakitarajia mgogoro kuibuka mwishoni mwa wiki, huku wakibaini dalili za wasiwasi kutoka Israel kuhusu ukubwa wa mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka Iran. Katika siku za hivi karibuni, imebainika kuwa Trump anataka kudhibiti si tu mabaki ya mpango wa nyuklia wa Iran uliodhoofika, bali pia uwezo wa Iran kurusha makombora ya masafa marefu, ambayo kwa muda mrefu yameonekana kama msingi wa nguvu ya kijeshi ya Tehran. Aidha, Trump pia amependekeza kuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, aondoke kwenye ulingo wa dunia, dai ambalo Iran imelipinga vikali. Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei. Baadhi ya wachambuzi wanaona kuongezeka ghafla kwa vitisho hivyo kama njia ya kuvuruga tahadhari ya umma, wakati Trump anakabiliwa na shinikizo la kisiasa la ndani kufuatia vitendo vya vurugu vilivyofanywa na maafisa wa usalama wa ndani katika jimbo la Minnesota. Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema hatakuwa tayari kufanya mazungumzo chini ya vitisho, lakini yuko tayari kujadiliana bila masharti, msimamo ambao amesema umefikishwa kwa Trump kupitia wapatanishi kadhaa kwa mjumbe maalum wa Marekani, Steve Witkoff. MBUNGE ILHAN OMAR ASHAMBULIWA WAKATI AKIHUTUBIA – AMWAGIWA MAJIMAJI – POLISI WAINGILIA KATI USA

Share this post: