Stanbic Yaandaa Futari Kuimarisha Mahusiano na Wadau
2026-03-12 - 14:38
Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ally na Omari Mtiga, Mkuu wa Wateja Binafsi na Wateja Maalum wa benki ya Stanbic Wakijipakulia Futari Benki ya Stanbic imeandaa futari maalum iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, ikiwa ni sehemu ya kushiriki baraka za mwezi mtukufu wa Ramadan pamoja na kuimarisha mahusiano na wadau wake. Tukio hilo liliwakutanisha viongozi wa dini, viongozi wa benki pamoja na wateja katika mazingira ya mshikamano na tafakari ya maadili ya kijamii yanayohimizwa katika kipindi hiki cha Ramadhani. Wafanyakazi wa Stanbic Kwenye Futari Iliyoandaliwa na Benki Hiyo Jijini Dar es saalam. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ally, huku ujumbe wa Stanbic Bank ukiongozwa na Omari Mtiga, Mkuu wa Wateja Binafsi na Wateja Maalum wa benki hiyo. Kupitia futari hiyo, Stanbic Bank ilisisitiza dhamira yake ya kuendelea kujenga mahusiano ya karibu na wadau wake huku ikiendeleza maadili ya heshima, mshikamano na utoaji kwa jamii. Tukio hilo pia lilitoa fursa kwa washiriki kubadilishana mawazo na kuimarisha ushirikiano unaochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.