TheTanzaniaTime

Sowah Hatihati Kutimuliwa Simba Kwa Utovu wa Nidhamu

2026-03-17 - 13:44

MSHAMBULIAJI namba moja wa Simba, Jonathan Sowah kuna hatihati kuondoka ndani ya kikosi hicho kutokana na tatizo la nidhamu. Sowah ndani ya NBC Premier League amefunga magoli matatu akiwa ni miongoni mwa wachezaji wenye magoli mengi ndani ya kikosi hicho. Kwa sasa Sowah hayupo kwenye mipango ya timu hiyo kutokana na kile kilichoelezwa alisimamishwa na uongozi kutokana na masuala ya nidhamu. Alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu katika mechi za ushindani baada ya kufungiwa mechi 5 na hata adhabu yake ilipoisha hakurejea uwanjani kwa mechi za ushindani isipokuwa Kante alirejea na kuendelea na mechi za ushindani. Taarifa zinaeleza kuwa Sowah aliyesajiliwa na Simba SC akitokea Singida Black Stars aliondolewa wakati kikosi kikiwa kambini Zanzibar kwa maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Yanga SC uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex wakigawana pointi mojamoja kwa kutokufungana. Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.

Share this post: