Simba Yatoa Tamko Baada ya Kukwama Kutinga Robo Fainali CAF
2026-02-03 - 06:10
UONGOZI wa Simba umewaomba mashabiki kutokata tamaa wala kuivunjia adabu timu hiyo mara baada ya matumaini ya kukata tiketi kutinga hatua ya robo fainali kuzimika Februari Mosi 2026. Sare ya kufungana magoli 2-2 de Tunis inainfanya Simba SC kukusanya pointi moja baada ya mechi nne ikiburuza mkia katika kundi D. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram amewaomba mashabiki kutokata tamaa; Ujumbe huu hapa: “Tusife moyo wala tusiingie unyonge ndugu zangu Wanasimba kushindwa kufanya vizuri kimataifa msimu huu isitunyongonyeshe bali itupe nguvu ya kujipanga msimu ujao, “Wakati mwingine ili ufike juu lazima uanzie chini, Msimu huu tumeteleza lakini tusiivunjie adabu timu yetu ambayo imetupa heshima kubwa Afrika. “Nafahamu wasiotutakia mema watajaribu kunadi kufeli kwetu msimu huu kuwa ni tatizo kubwa ambalo halijawahi kutokea duniani lengo ni kuchonganisha mashabiki na timu yao mashabiki na viongozi wao. “Wakati huu na tuchague cha kusikiliza na tuchague cha kuongea wengi wanaonekana kama wanaipigania klabu au wanatutetea lakini uhalisia wanachochea vurugu klabuni kwetu. “Tuilinde nembo ya klabu yetu... Mnyama atarejea tuu kwenye ufalme wake tena hivi punde tuu,”. Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.