Simba Yapoteza Imani ya Mashabiki Uwanja wa Benjamin Mkapa – Video
2026-02-13 - 02:20
Msemaji wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema timu hiyo imepata matokeo mabaya katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kusababisha mashabiki wapoteze imani na ule msemo kwamba ‘Kwa Mkapa hatoki Mtu’. Amesema katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Stade Malien, japokuwa hata wakishinda hawataenda popote, wanataka kuutumia mchezo huo kulinda heshima ya Simba na kurudisha imani kwa mashabiki. Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
Share this post: