TheTanzaniaTime

Shilole Awaacha Mashabiki Vinywa Wazi kwa Ujumbe wa Kimahaba

2026-02-14 - 04:30

Msanii wa filamu za Bongo Muvi na mjasiriamali anayemiliki mgahawa maarufu wa Shishi Food, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameonyesha upande wake wa kimahaba baada ya kushiriki ujumbe mzito uliojaa mapenzi na hisia kwa mashabiki wake. Kupitia maneno yenye mvuto na mahaba, Zuwena amesema: “Uwanja wa Mapenzi nimeufungua! Leo tunafungua rasmi Uwanja wa Mapenzi – mahali ambapo hisia zinang’aa. Mimi na shemeji yenu tunashirikiana katika moment hii ya kipekee, ambapo kila tabasamu, kila mguso, na kila anguko la mwanga linazungumza hadithi yetu ya mapenzi. Hii si safari ya kawaida... hii ni experience yetu ya mapenzi, mahaba yanayowasha hisia, na kila sekunde ni magic. Nampenda sana huyu Baba . Nitarudi na hadithi fupi .” Ujumbe huo umeibua gumzo mitandaoni, mashabiki wengi wakimpongeza kwa kuonesha furaha ya moyo na kuthamini mapenzi hadharani. Wengine wamesema ni “goals” halisi za maisha ya ndoa na mahusiano yenye amani. Mbali na sanaa, Zuwena amekuwa akifanya vizuri pia kibiashara kupitia mgahawa wake wa Shishi Food, jambo linalomfanya kuwa mfano wa mwanamke anayechanganya kazi, mafanikio na mapenzi kwa wakati mmoja.

Share this post: