Shigongo Awahimiza Vijana Kujiamini na Kutumia Vipaji vyao Kujiletea Maendeleo – Video
2026-02-13 - 08:59
Mbunge wa Buchosa na Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo. Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, amewataka vijana wa Kitanzania kujiamini na kuthamini vipaji walivyopewa, akisisitiza kuwa kila mmoja ana uwezo wa kubadilisha maisha yake na jamii inayomzunguka. Akizungumza jana kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za Tanzania Creator Awards, Shigongo alisema vijana wengi wanashindwa kufikia mafanikio si kwa kukosa vipaji, bali kwa kukosa kujiamini na kuthubutu. “Mungu tayari ameweka karama na kipaji ndani yako. Kazi yako ni kuvitambua, kuvikuza na kuvitumia kutatua changamoto za jamii,” alisisitiza Shigongo. Aliongeza kuwa zama za sasa zinahitaji ubunifu, teknolojia na uthubutu, akiwahimiza vijana kutumia akili zao na vipaji vyao kuanzisha miradi, biashara na suluhisho bunifu badala ya kusubiri ajira pekee. Katika hafla hiyo, Shigongo pia alitunukiwa Tuzo ya Heshima (Lifetime Recognition Award) kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya Printing and Digital Media, akitambuliwa kwa juhudi zake za kukuza tasnia ya uchapishaji, uandishi na vyombo vya habari vya kidijitali nchini. Washiriki wa tukio hilo walimpongeza kwa kuwa mfano wa kuigwa, wakieleza kuwa safari yake ya ujasiriamali na media imewapa motisha vijana wengi kuamini ndoto zao. View this post on Instagram A post shared by globalpublishers (@globaltvonline)