TheTanzaniaTime

Shabbiy Bus Yafanya Maboresho Makubwa ya Vyoo na Kituo Kikuu cha Upakiaji Abiria Dodoma

2026-02-20 - 15:07

Kampuni ya mabasi Shabbiy Bus imefanya maboresho makubwa ya vyoo katika Kituo Kikuu cha Upakiaji Abiria jijini Dodoma, ambavyo awali vilikuwa katika hali ya uchakavu, hatua inayolenga kuboresha mazingira na ustawi wa wasafiri. Mbali na marekebisho hayo, kampuni hiyo inaendelea na ukarabati mkubwa wa kituo hicho ili kuhakikisha abiria wanapata huduma bora na za kisasa. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kampuni hiyo, ujenzi wa jengo kubwa la kupumzikia abiria pamoja na mgahawa mkubwa wa chakula unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Hatua hizi ni sehemu ya mkakati wa kampuni ya Shabbiy Bus kuboresha miundombinu na kuinua viwango vya huduma katika sekta ya usafiri wa abiria, hususan katika mji wa Dodoma ambao ni kitovu cha shughuli za kitaifa. Maboresho hayo yanatarajiwa kuongeza faraja, usalama na kurahisisha safari kwa maelfu ya abiria wanaotumia kituo hicho kila siku.

Share this post: