SBL Na Wizara Ya Fedha Mambo Safi, Kuimarisha Ukuaji Uchumi Nchini
2026-03-04 - 19:17
Naibu Waziri wa Fedha, Eng. Mshamu Ali Munde katika kikao na Uongozi Wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), imekutana na Naibu Waziri wa Fedha, Eng. Mshamu Ali Munde katika kikao kikubwa kilicholenga kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi. Lengo ni kudumisha uthabiti wa biashara na kuongeza kasi ya ukuaji wa Uchumi wa Tanzania. Uongozi wa SBL uliokuwa kando na Mwenyekiti wa Bodi, Paul Makanza, na Mkurugenzi Mtendaji, Obinna Anyalebechi uliongoza mazungumzo hayo. Kama moja ya wazalishaji wakuu nchini Tanzania, SBL imewekeza zaidi ya shilingi 165 bilioni katika shughuli zake za ndani katika miaka ya hivi karibuni ikionesha dhamira yake ya kudumu katika uzalishaji wa ndani na ukuaji wa viwanda. Kampuni hiyo inachangia zaidi ya shilingi 220 bilioni kila mwaka katika uchumi wa taifa na ina ushiriki wa zaidi ya 33% katika soko la vinywaji. SBL inaendelea kuwa mchangiaji muhimu wa mapato ya serikali, upanuzi wa uzalishaji wa ndani na kuimarisha minyororo ya thamani ya Tanzania. Zaidi ya utengenezaji wa bia, SBL inawekeza shilingi 15 bilionsssi kila mwaka katika minyororo yake ya usambazaji wa ndani, ikinunua karibu tani 20,000 za nafaka zinazolimwa nchini. Uwekezaji huo endelevu unakuza minyororo ya thamani ya kilimo, unaunga mkono wakulima maelfu, unakuza uzalishaji wa ndani na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje. Pia inaunga mkono ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 800 huku ikirahisisha maisha ya zaidi ya watu 140,000 kupitia minyororo yake ya thamani – kuanzia wakulima, wasambazaji, wauzaji hadi wawekezaji wa hoteli na baa. Mazungumzo kwenye kikao hicho yalizingatia umuhimu wa kudumisha mazingira ya kifedha na kisheria thabiti na yanayoweza kutabirika ili kuhimiza uwekezaji wa muda mrefu wa sekta binafsi, kuimarisha uwezo wa viwanda vya ndani, kuongeza ununuzi wa bidhaa za ndani na kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi kwa ukuaji wa uchumi unaojumuisha na endelevu. Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji Obinna Anyalebechi alisema: “Kampunia ya Bia ya Serengeti imejikita kwenye hadithi ya ukuaji wa Tanzania. Uwekezaji wetu hauishii kwenye utengenezaji tu, bali unaimarisha viwanda vya ndani, unapanua msingi wa kodi, unaunga mkono wakulima, unaajiri na kujenga minyororo imara ya thamani. Mazingatio ya biashara thabiti na yanayoweza kutabirika ni muhimu kwa uwekezaji wa muda mrefu na tutaendelea kushirikiana kwa karibu na serikali kuendesha maendeleo ya uchumi endelevu.” Naye Naibu Waziri wa Fedha Eng. Mshamu Ali Munde alibainisha: “Sekta binafsi ina nafasi muhimu katika mabadiliko ya uchumi wa Tanzania. Kulingana na Dira ya Maendeleo ya Taifa, serikali imeweka lengo la kujenga uchumi wa dola trilioni moja ifikapo 2050, ambapo takriban asilimia 70 ya ukuaji huu unatarajiwa kuendeshwa na sekta binafsi. Michango ya Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia kodi, uwekezaji wa viwanda na miradi ya kijamii inastahili pongezi. Serikali inaendelea kujitahidi kuunda mazingira yanayofaa kwa biashara na uwekezaji na tutaendelea kushirikiana katika mapendekezo yaliyotolewa ili kuimarisha ushirikiano wa umma na sekta binafsi na kuboresha urahisi wa kufanya biashara kwa wawekezaji, kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.” Kampuni ya Bia ya Serengeti, imesisitiza dhamira yake ya kushirikiana na Wizara ya Fedha kukuza viwanda, kupanua minyororo ya thamani ya ndani na kuchangia katika mabadiliko ya uchumi wa Tanzania kwa muda mrefu, sambamba na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.