TheTanzaniaTime

Rais Samia Kushiriki Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi za EAC leo Arusha

2026-03-07 - 07:07

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu pamoja pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha . CPA. Amos Makalla na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), tarehe 06 Machi, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kushiriki katika Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika leo Machi 7, 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Rais Samia aliwasili Machi 6, 2026 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo alipokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wananchi. Mara baada ya kuwasili, Rais Samia alipata burudani ya utamaduni kutoka kwa kikundi cha sanaa cha Maasarie Troupe kilichowasilisha ngoma na maonesho ya kitamaduni kumkaribisha. Mkutano huo muhimu wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unatarajiwa kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Mkutano huo utakutanisha Wakuu wa Nchi wanachama wa EAC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kikanda, maendeleo ya kiuchumi pamoja na kuimarisha mshikamano wa nchi wanachama. Viongozi wa nchi za EAC wanatarajiwa kujadili pia hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya pamoja ya maendeleo, biashara ya kikanda, miundombinu pamoja na masuala ya amani na usalama ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki. MAKOMBORA HATARI ya IRAN YALIVYOIPIGA ISRAEL na WANAJESHI wa MAREKANI – VITA INAENDELEA...

Share this post: