TheTanzaniaTime

Rais Samia Aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Matanki ya Mafuta Kigamboni (Picha +Video)

2026-03-03 - 12:28

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Matanki ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam katika eneo la Kigamboni Mnadani Jijini Dar es Salaam, tarehe 03 Machi, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Machi 3, 2026 ameongoza hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi wa ujenzi wa matanki ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, eneo la Kigamboni Mnadani. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wageni mashuhuri. Mradi huu ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha miundombinu ya nishati na kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa uhakika nchini. Matanki haya yatasaidia kupunguza muda meli zinavyosubiri kuingia bandari kutoka wastani wa siku 22 hadi siku 7, pamoja na kupunguza muda wa kushusha shehena ya mafuta kutoka siku 7 hadi siku 1. Aidha, mradi huu unatarajiwa kuongeza mapato ya Taifa kupitia tozo na huduma za bandari, sambamba na kutoa ajira kwa Watanzania katika hatua za ujenzi na uendeshaji. Ujenzi wa matanki haya pia unalenga kupunguza changamoto za uhaba wa mafuta na kuongeza ufanisi wa usambazaji wake katika sekta ya nishati. Rais Samia amesisitiza kuwa mradi huu ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa na unaonyesha dhamira ya Serikali katika kuhakikisha miundombinu ya kimkakati inakidhi mahitaji ya wananchi. Rais Samia akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Matanki ya kupokea mafuta. Muonekano wa eneo la Mradi wa ujenzi wa Matanki ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa Matanki hayo utasaidia kupunguza au kuondoa kabisa uhaba wa mafuta Nchini, kuimarisha usalama wa nishati hiyo, kupunguza muda wa meli kusubiri nangani kutoka wastani wa siku 22 hadi siku 7, kupunguza muda wa kushusha shehena ya mafuta kutoka siku 7 hadi siku 1, kuongeza mapato ya Taifa kupitia makusanyo ya kodi na tozo mbalimbali zitakazo kusanywa na Mamlaka husika pamoja na kutoa ajira kwa Watanzania.

Share this post: