TheTanzaniaTime

Rais Samia Awasili Dubai, Azungumza na Waziri wa Sheria – Video

2026-02-02 - 19:29

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Maktoum (DWC), Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Februari 02, 2026. Mara baada ya kuwasili, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alifanya mazungumzo na Waziri wa Sheria wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Abdullah bin Sultan bin Awad Al Nuaimi, katika uwanja huo wa ndege. Katika ziara hiyo, Rais Dkt. Samia atashiriki katika Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit – WGS) 2026, pamoja na kushiriki Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji Afrika (Global Africa Investment Summit – GAIS), linalolenga kukuza ushirikiano wa kiuchumi na uwekezaji kati ya Afrika na dunia.

Share this post: