Rais Samia Apanda mti Bungi Kilimo, Zanzibar kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa – Video
2026-01-27 - 10:22
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi mara baada ya kuongoza Zoezi la kupanda miti kwenye eneo la Bungi Kilimo,Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 27 Januari, 2026, wakati wa kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa. Rais Samia Suluhu Hassan akikata Keki mara baada ya kuongoza upandaji miti kwenye eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Unguja leo tarehe Januari 27, 2026, wakati wa kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amepanda mti katika eneo la Bungi Kilimo, Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa. Mti huo ambao ni wa aina ya Mangifera indica kitaalamu, unaofahamika kwa jina la Mwembe Shomari, umepandwa leo Januari 27, 2026 tarehe ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais Samia. Tukio hilo limefanyika sambamba na Kampeni ya 27 ya Kijani, inayolenga kuhamasisha upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira ili kuifanya Tanzania kuwa ya kijani.