TheTanzaniaTime

Rais Samia Afanya Mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed

2026-02-14 - 08:10

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika, tarehe 14 Februari, 2026 jijini Addis Ababa, Ethiopia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), tarehe 14 Februari 2026, jijini Addis Ababa, Ethiopia. Katika kikao hicho, viongozi hao wawili walijadili masuala ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili kati ya Tanzania na Ethiopia, hususan katika sekta za biashara, uwekezaji, miundombinu, nishati na usafiri wa anga. Aidha, waligusia umuhimu wa mshikamano wa bara la Afrika katika kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kijamii, sambamba na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati kupitia ajenda za Umoja wa Afrika. Mazungumzo hayo yanaashiria dhamira ya mataifa hayo mawili kuendelea kukuza uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wake pamoja na maendeleo ya bara zima la Afrika.

Share this post: