Rais Dkt. Samia Aondoka Addis Ababa Baada ya Kushiriki Mkutano wa AU
2026-02-15 - 11:01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiondoka Kiwanja che Ndege cha Kimataifa cha Bole, Addis Ababa, nchini Ethiopia kurejea nchini Tanzania, leo tarehe 15 Februari, 2026. Rais Dkt. Samia alikuwemo nchini humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne, ambapo pamoja na mambo mengine alishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika tarehe 14 na 15 Februari, 2026.
Share this post: