TheTanzaniaTime

Pope Leo XIV Aponda Vita Jumapili ya Matawi ‘Mungu Hahusiki na Mauaji’

2026-03-29 - 10:55

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Pope Leo XIV, amekataa vikali madai kwamba dini au Mungu vinaweza kutumika kuhalalisha vita, akisisitiza kuwa Mungu ni Mfalme wa Amani anayekataa vurugu na mateso. Akihutubia maelfu ya waumini katika misa ya Jumapili ya Matawi (Palm Sunday) iliyofanyika katika St. Peter’s Square, leo Machi 29, 2026 kiongozi huyo aliweka wazi msimamo wa Kanisa dhidi ya matumizi ya dini katika migogoro ya kivita. “Yesu ni Mfalme wa Amani anayekataa vita, na hakuna anayeweza kumtumia kuhalalisha vita,” alisema. Kauli ya Papa imekuja wakati dunia ikiendelea kushuhudia migogoro mikubwa, ikiwemo vita kati ya Iran na Israel pamoja na vita ya Russia dhidi ya Ukraine. Katika hotuba yake, Pope Leo XIV alionya dhidi ya viongozi wanaotumia imani zao kuhalalisha mapigano, akisema Mungu hasikilizi maombi ya wanaoanzisha vita bali huwafariji wanaoteseka. Papa alitoa pia maombi maalum kwa Wakristo wanaoishi katika Middle East, akisema wengi wao wanateseka kutokana na migogoro na kushindwa kushiriki kikamilifu ibada muhimu za kipindi cha Pasaka. Aidha, alisisitiza kuwa mateso ya watu katika maeneo ya vita yanapaswa kugusa dhamiri za dunia nzima na kuhimiza juhudi za kweli za maridhiano na amani. Palm Sunday huashiria mwanzo wa Wiki Takatifu, kipindi muhimu kwa Wakristo kinachokumbuka mateso, kusulubiwa na kufufuka kwa Yesu Kristo, kinachohitimishwa na Easter Sunday. Katika kipindi hiki, Papa Leo XIV amewataka waumini kutafakari mateso ya watu duniani wanaopitia hali ngumu kama ile aliyopitia Kristo, na kuongeza juhudi za kuleta amani.

Share this post: