TheTanzaniaTime

Polisi Inawasaka Waliomrekodi Mtoto Akivuta Sigara

2026-02-15 - 10:50

Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi baada ya kusambaa kwa picha mjongeo mtandaoni inayomuonesha mtoto mdogo wa kiume akihamasishwa kuvuta sigara. Polisi wamesema tukio hilo ni kinyume cha sheria na maadili ya jamii, na kwamba wanaendelea kuwafuatilia waliohusika ili wachukuliwe hatua za kisheria. Aidha, wametoa wito kwa wananchi wenye taarifa kuhusu tukio hilo kusaidia uchunguzi. Onyo pia limetolewa kwa watu wanaotumia watoto kutengeneza maudhui ya mitandao ya kijamii kwa namna inayoweza kuhatarisha afya au ustawi wao kuacha mara moja, huku wakisisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa watakaobainika .

Share this post: