Pingamizi la Said Issa Mohammed Dhidi ya Lissu Latupiliwa Mbali
2026-03-03 - 07:28
Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imeyatupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na Said Issa Mohammed na wenzake kupinga Lissu kuunganishwa katika Kesi ya Mgawanyo wa Mali inayowakabili Katibu Mkuu wa CHADEMA na Bodi ya Wadhamini. Uamuzi huo umetolewa na Jaji Hamidu Mwanga leo Machi 03, 2026 baada ya kutupilia mbali mapingamizi mawili yaliyowekwa na Wakili wa walalamikaji (Said Issa Mohammed na Wenzake) Kwa msingi huu maombi ya msingi ya Lissu yatasikilizwa Ijumaa ya Machi 06, 2026 saa tatu asubuhi mbele ya Jaji Hamidu Mwanga.
Share this post: