Picha: Rais Samia Akipokea Ripoti ya CAG, TAKUKURU na PPRA
2026-03-30 - 12:15
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu akipokea ripoti mbalimbali kutoka taasisi za umma katika Ikulu ya Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Machi 30, 2026, amepokea ripoti mbalimbali kutoka taasisi za umma katika Ikulu ya Dar es Salaam. Ripoti zilizowasilishwa mbele ya Rais ni pamoja na ile ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Matukio hayo yameoneshwa kupitia picha mbalimbali zikimuonesha Rais Samia akipokea na kukabidhiwa ripoti hizo kutoka kwa viongozi wa taasisi husika.
Share this post: