Picha 15 za Safari ya Mwisho ya Lukuvi Kutoka Dodoma mpaka Dar, Kuagwa Rasmi leo
2026-03-28 - 08:06
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), marehemu William Lukuvi, ulivyowasili jijini Dar es Salaam Machi 27, 2026 na kupelekwa nyumbani kwake Mbezi Beach kwa ajili ya maandalizi ya kuaga rasmi. Baada ya kuwasili, mwili huo ulipelekwa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Gasper De Bufallo ambapo ulifanyiwa ibada maalum ya kumuombea marehemu, ikiwa ni sehemu ya taratibu za mwisho kabla ya mazishi. Awali, mwili wa marehemu Lukuvi ulitolewa jijini Dodoma kufuatia shughuli ya kuuaga iliyofanyika katika Viwanja vya Bunge tarehe 27 Machi, 2026, ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali na wabunge walitoa heshima zao za mwisho. Ratiba inaonesha kuwa mwili huo utaagwa rasmi kesho, leo Machi 28, 2026 katika Viwanja vya Karimjee, ambapo wananchi wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo. Marehemu Lukuvi alifariki dunia tarehe 25 Machi, 2026 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.