Nyota ya Leicester Alisha Lehmann Aonyesha Gari Jipya ‘Batman’ Ya Mil 400
2026-02-19 - 04:06
Mchezaji wa soka wa kimataifa ya wanawake ya Swiss na Leicester City, Alisha Lehmann, amewaacha midomo wazi mashabiki wake baada ya kuonyesha gari lake jipya linalofanana na “Batmobile” linalodaiwa kuwa na thamani ya takribani pauni 130,000 (Tsh 455,204,230). Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye amewahi kutajwa mara kadhaa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na mvuto wake na umaarufu wake uwanjani, alihama kutoka klabu ya Como katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari na kujiunga na Leicester. Mercedes Yageuzwa Kuwa “Batmobile” Gari hilo ni Mercedes-Benz GLE Coupe AMG, ambalo awali lilikuwa na rangi nyeupe inayong’aa kabla ya kubadilishwa rangi kuwa nyeusi ya matte inayotoa mwonekano mkali na wa kifahari zaidi. Licha ya kubadili mazingira kutoka Como kwenda Leicester, inaonekana hakuna kilichobadilika kuhusu mtindo wa maisha wa kifahari wa Lehmann. Gari hilo linaongezeka kwenye mkusanyiko wake wa magari ya thamani, jambo linaloonyesha mafanikio yake ndani na nje ya uwanja. Lehmann ameendelea kujenga jina lake si tu kama mchezaji wa soka, bali pia kama sura maarufu kwenye mitandao ya kijamii, akiwa na mamilioni ya wafuasi wanaofuatilia maisha yake ya kila siku.