TheTanzaniaTime

Nafasi 08 za Ajira Zatangazwa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

2026-02-22 - 05:06

Halmashauri ya Wilaya ya Kyela imetangaza nafasi nane (08) za ajira baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Soma zaidi hapa>>>NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA Nafasi Zilizotangazwa 1⃣ Dereva Daraja la II – Nafasi 06 Majukumu: Kukagua gari kabla na baada ya safari Kuwapeleka watumishi safari za kikazi Kufanya matengenezo madogo ya gari Kusambaza nyaraka Kujaza daftari la safari Kufanya usafi wa gari Kazi nyingine atakazopangiwa Sifa: Elimu ya Kidato cha Nne Leseni Daraja C au E Uzoefu wa angalau mwaka mmoja bila kusababisha ajali Cheti cha Basic Driving Course kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa Mshahara: TGS B 2⃣ Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 02 Majukumu: Kuchapa barua na nyaraka (za kawaida na siri) Kupokea na kuwaelekeza wageni Kutunza kumbukumbu za ofisi Kupanga majalada na maandalizi ya vikao Kuandaa mahitaji ya vifaa vya ofisi Kazi nyingine atakazopangiwa Sifa: Kidato cha Nne Stashahada (NTA Level 6) ya Uhazili Ujuzi wa Shorthand (80 w.p.m) Kiswahili na Kiingereza Ujuzi wa kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher) Mshahara: TGS C Masharti ya Jumla Mwombaji awe raia wa Tanzania (miaka 18–45) CV kamili na wadhamini watatu Vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili Waombaji waliostaafu au watumishi wa umma wafuate taratibu maalum Vyeti vya nje ya nchi vithibitishwe na TCU/NACTE/NECTA Maombi ya kughushi hayatavumiliwa Mwisho wa kupokea maombi: 05 Machi, 2026 Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa Ajira (Recruitment Portal): https://portal.ajira.go.tz/ Barua ielekezwe kwa: Mkurugenzi Mtendaji (W) Halmashauri ya Wilaya ya Kyela S.L.P 320, Kyela – Mbeya

Share this post: