TheTanzaniaTime

Mwili wa Lukuvi Waagwa Iringa Kabla ya Mazishi Idodi Kesho (Picha +Video)

2026-03-30 - 09:24

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi, umefikishwa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Kanisa Kuu – Kihesa, Jimbo Katoliki Iringa, ukitokea nyumbani kwake Gangilonga Manispaa ya Iringa leo Machi 30, 2026. Mwili huo umepelekwa Kihesa kwa ajili ya Ibada Maalum na shughuli ya kuaga, ambapo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, ndugu, jamaa na wananchi wanatarajiwa kujitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Lukuvi. Baada ya kukamilika kwa ibada na zoezi la kuaga, mwili wa William Lukuvi utasafirishwa kuelekea Kijiji cha Idodi kilichopo Iringa Vijijini, ambako maziko yatafanyika kesho Machi 31, 2026. Shughuli za heshima za mwisho zinaendelea kufanyika kwa utaratibu maalum, zikihitimisha safari ya marehemu Lukuvi ambaye alihudumu katika nyadhifa mbalimbali serikalini na bungeni.

Share this post: