TheTanzaniaTime

Mwigulu Atumia SGR Kuelekea Morogoro Kufungua Mkutano wa TAKUKURU

2026-01-26 - 06:47

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Januari 26, 2026, ameondoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Morogoro kwa kutumia Treni ya Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR). Katika safari hiyo, Dkt. Mwigulu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Mwaka wa Viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa TAKUKURU kutoka maeneo mbalimbali nchini, ukiwa na lengo la kutathmini utekelezaji wa majukumu yao, kubadilishana uzoefu, pamoja na kuweka mikakati ya kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Share this post: