Mwanaheri Atoa Ujumbe Mzito Baada ya Kuolewa ‘Bwana nnae na natamba nae’
2026-02-02 - 03:39
Msanii wa Bongo Movie, Mwanaheri maarufu kwa jina la Madam Simba, amefunguka kwa furaha baada ya kuolewa rasmi, tukio lililowagusa mashabiki wake wengi kwenye mitandao ya kijamii. Kupitia ujumbe aliouchapisha, Mwanaheri alieleza hisia zake kwa maneno yaliyojaa shukrani na furaha, akisisitiza umuhimu wa imani na dua katika safari ya maisha yake. “Kila hatua dua Mr and Mrs Said, tupo lelelele Bwana nnae na bwana natamba nae,” ameandika Mwanaheri. Ujumbe huo umeibua pongezi nyingi kutoka kwa mashabiki, wasanii wenzake pamoja na wadau wa burudani, wakimtakia heri na baraka katika maisha mapya ya ndoa. Madam Simba ni miongoni mwa wasanii waliodumu kwa muda mrefu katika tasnia ya filamu nchini, akitambulika kwa uigizaji wake wenye mvuto na mchango wake mkubwa katika Bongo Movie. Ndoa yake imeendelea kuwa gumzo mitandaoni, huku wengi wakifurahia kumuona msanii huyo akipata furaha na utulivu katika maisha yake binafsi.