Mwalimu wa Kiingereza wa Diamond, Allen Ngonyani Afariki Dunia
2026-03-15 - 10:58
Mwalimu aliyewasaidia mastaa wakubwa wa muziki wa Bongo Fleva, akiwemo Diamond Platnumz, Harmonize na Rayvanny, kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha, Allen Ngonyani, amefariki dunia mapema asubuhi ya leo katika Hospitali ya Geza, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu. Akizungumza na Global TV Online, mmoja kati ya ndugu wa karibu wa marehemu amesema kuwa Ngonyani alilazwa hospitalini hapo kwa siku mbili kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu uliokuwa unamsumbua. Ameongeza kuwa familia kwa sasa inaendelea kufanya mawasiliano na ndugu wengine waliopo Songea ili kupanga taratibu za mazishi.
Share this post: