TheTanzaniaTime

Mtoto Darasa la 4 Afariki kwa Kuzama Mtoni Iringa – Video

2026-02-05 - 15:28

Hali ya huzuni na simanzi imetanda miongoni mwa wakazi wa Mtaa wa Kitwiru, Manispaa ya Iringa, kufuatia kifo cha mtoto Geofrey Malate (11), aliyefariki dunia baada ya kuzama katika Mto Ruaha Mdogo. Kwa mujibu wa mzazi na mashuhuda wa tukio hilo, Geofrey, mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Kilonga A, alipata ajali hiyo wakati akijaribu kuogelea katika mto huo, lakini alishindwa kumudu kasi ya maji na hatimaye kuzama hadi kupoteza maisha.

Share this post: