Mirambo Ashinda Kwa Kishindo Uenyekiti CUF, Achukua Nafasi Ya Prof. Lipumba
2026-02-22 - 10:06
Chama cha Wananchi (CUF) kimempata Mwenyekiti mpya wa Taifa, ambapo Mirambo Camil Yusuf amechaguliwa kushika nafasi hiyo akichukua mikoba ya Ibrahim Lipumba, aliyekuwa akiiongoza tangu mwaka 1999. Matokeo hayo yametangazwa Februari 22, 2026 na Mwenyekiti wa Uchaguzi wa chama hicho, Said Miraji, baada ya mkutano mkuu wa dharura uliohudhuriwa na wajumbe 456. Matokeo ya Uenyekiti Taifa Mirambo Camil Yusuf – Kura 257 Othman Omar Dunga – Kura 177 Nkunyunyika Siwale – Kura 6 Jumla ya kura halali zilikuwa 448 huku kura 6 zikiharibika. Mirambo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Kigoma Mjini, sasa ataongoza chama hicho katika kipindi kipya cha uongozi. Matokeo Mengine Makamu Mwenyekiti Bara Miraji Mtibwiliko – Kura 264 Mohammed Ngulangwa – Kura 88 Mussa Mbarouk – Kura 82 Makamu Mwenyekiti Zanzibar Haroub Mohamed Shamsi – Kura 256 Mbarouk Seif Salim – Kura 171 Amina Rashid Salim – Alijitoa Uchaguzi huo umeashiria mabadiliko makubwa ya uongozi ndani ya CUF baada ya takribani miongo miwili chini ya Profesa Lipumba.