Mchumba wa Marehemu Irene Robert Akamatwa Hospitali ya Mwananyamala
2026-03-27 - 08:24
Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Irene Robert enzi za uhai wake. Mchumba wa marehemu anayefahamika kwa jina la Irene Robert, maarufu kwa jina la Brian Mutenye Waboto, anadaiwa kukamatwa na jeshi la polisi akiwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa za awali, Brian alikamatwa akiwa hospitalini hapo huku chanzo cha kukamatwa kwake kikiwa bado hakijafahamika wazi mara moja. Polisi wamechukua hatua hiyo kama sehemu ya ufuatiliaji wa tukio linalohusiana na kifo cha Irene Robert, ambapo uchunguzi unaendelea ili kubaini ukweli wa kilichotokea. Mashuhuda waliokuwepo hospitalini wamesema polisi waliowasili na kumchukua mtuhumiwa huyo bila kutokea vurugu kubwa. Hata hivyo, hakukuwa na taarifa rasmi zilizotolewa mara moja na mamlaka husika kuhusu tuhuma zinazomkabili au hatua zinazofuata. Polisi wamesema wataendelea kutoa taarifa rasmi mara uchunguzi utakapokamilika na ukweli zaidi utakapopatikana kuhusu mazingira ya tukio hilo. Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Irene Robert, amefariki Machi 20, 2026 baada ya kuugua ghafla.