Mbunge Shigongo Apongeza Maboresho ya Afya chini ya Rais Samia – Video
2026-03-16 - 17:17
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, amesema kuwa ameridhishwa na juhudi za serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya nchini, ikiwemo maboresho makubwa yanayofanywa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shigongo aliyasema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge katika hospitali hiyo, akisisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kumuunga mkono Rais Samia, kwa sababu serikali yake inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya. “Ni wazi kuwa serikali inatilia mkazo sana afya za wananchi, na maboresho haya yanayofanywa Muhimbili ni ishara tosha ya dhamira ya Rais Samia ya kuboresha sekta ya afya nchini,” amesema Shigongo. Ziara ya Kamati ya Bunge ililenga kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya afya na kuhakikisha rasilimali zinazopatikana zinatumika ipasavyo kwa manufaa ya wananchi.