Mbunge Musukuma ‘Azichapa’ na Mwekezaji, Serikali Yatajwa Kuchukua Hatua – Video
2026-01-25 - 21:09
Wabunge kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita wameiomba serikali kuchukua hatua dhidi ya mwekezaji anayetuhumiwa kubomoa bila kibali majengo ya serikali katika kitongoji cha Katoro Center kilichopo mji mdogo wa Katoro. Wabunge hao ambao ni Joseph Musukuma wa Jimbo la Geita pamoja na Mhandisi Kija Ntemi wa jimbo la Katoro wamewasilisha malalamiko yao baada ya kamati ya Uchumi na fedha ya halmashauri kutembelea eneo hilo ambapo kuliibuka mzozo uliosababisha Musukuma ‘kuzichapa kavukavu’ na mwekezaji huyo. Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
Share this post: