Mbeto: Siku 100, Siyo Penalti Ya Mwisho Kwa Rais Samia, Ampa Tano Rais Mwinyi
2026-02-13 - 08:40
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Utikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis. KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Utikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, amesema Mafanikio katika kuwaletea wananchi maendeleo katika awamu yake ya Sita ya Rais hayapimwi Kwa siku 100 za uwepo wake madarakani Kwani hiyo siyo penalti yake ya mwisho katika kuwatumikia wananchi. Katika mazungumzo yake na Global Tv Online hivi karibuni mwenezi Mbeto amewataka wananchi kuendelea kumwamini Rais Samia na kuunga mkono maono yake ya kuwafanya wananchi kupata maendeleo yatakayoacha alama hata atakapomaliza muda wake wa kuongoza nchi. “Siku 100, siyo hitimisho la mheshimiwa Rais, Kama mchezo ndiyo kwaza uko dakika za mwanzo, makubwa aliyofanya yanaonekana na kila mwenye macho chanya. “Aliyoahidi kuwafanya ndani ya siku 100, hakuna lililokwa, bima ya afya Kwa wote mchakato wake umeanza Kwa Kasi, mikopo Kwa vijana upon na vikwazo vinaondolewa kupitia wizara ya vijana aliyoiunda. “Utashi ya kuwepo Kwa malidhiano haujapoa, ndiyo maana imeundwa tume ya kuchunguza yaliyotokea Oktoba 29 ili ya toe taswira ya malidhiano yenyewe, miradi ya maendeleo inaenda Kwa kasi nchi nzima elimu, afya, huduma za kijamii zinaboreshwa uchwao,” Mbeto. Aliongeza kuwa Kama jamii itaungana nà Kasi ya Rais Samia na kuacha kusikiliza kelele za wasioitakia mema nchi yetu maendeleo yatapatikana Kwa kupitia malengo ambayo nchi imeyaweka. Kuhusu mafanikio ya Rais Hussein Ali Mwinyi aliyoyafikia katika kipindi çha uongozi wake yameonekana hata Kwa wasio na macho ya maendeleo. “Zanzibar inasonga Kwa Kasi, anayebisha aje aone, asiache kuja na picha za Zanzibar ya zamani, Leo kila Kona kuna fursa za watu kujipatia kipato, miradi mingi inatekelezwa, naamini Kasi hii ikiendelea Rais Mwinyi aravuka malengo hata kabla ya muda wake madarakani kumalizika,” Mbeto. Aidha amewataka Wazanzibari kuendelea kudumisha umoja na mshikamano wao bila kujali itikadi za kisiasa, kidini au kikabila. GLOBAL TV YAPATA TUZO ya ‘BEST ONLNE MEDIA 2025’ – CHEKI VAIBU UKUMBINI...