TheTanzaniaTime

Mashindano ya FIFA Series 2026 Kuanza Leo Rwanda, Stars Kukiwasha

2026-03-26 - 07:33

Mashindano ya kimataifa ya soka ya FIFA Series 2026 yanaanza rasmi leo Machi 26, 2026 jijini Kigali, huku Rais wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA), Fabrice Shema, akitangaza zawadi mbalimbali zitakazowania kuanzia kombe la ubingwa hadi tuzo ya mchezaji bora wa mashindano. FIFA Series ni mpango mpya wa kimataifa ulioanzishwa na FIFA ili kutoa nafasi zaidi kwa timu za taifa kucheza mechi za kimataifa hasa zile ambazo hupata nafasi chache ya kukutana na timu kutoka mabara mengine. Kuanzia leo, viwanja vya Amahoro na Kigali Pelé vinakuwa kitovu cha soka duniani, huku mataifa nane yakishuka dimbani yakisaka ushindi na kujijengea heshima kimataifa. Mashindano haya yanakusanya timu kutoka mabara tofauti, yakitoa nafasi kwa timu kujipima uwezo na kuongeza uzoefu wa kimataifa. Timu shiriki zimepangwa katika makundi mawili KUNDI A (Uwanja wa Amahoro) Rwanda (Wenyeji) Kenya Estonia Grenada KUNDI B (Uwanja wa Kigali Pelé) Tanzania (Taifa Stars) Liechtenstein Aruba Macau Mechi za leo (Machi 26): Tanzania Liechtenstein (Uwanja wa Kigali Pelé) Aruba Macau (Uwanja wa Kigali Pelé)

Share this post: