TheTanzaniaTime

Manchester United Yaifunga Tottenham 2-0, Yafikisha Ushindi wa Nne Mfululizo

2026-02-07 - 14:48

Manchester United, chini ya kocha Michael Carrick, wameendelea na mwendo wa ushindi katika Ligi Kuu England baada ya kuibuka na ushindi wa 2–0 dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa ligi uliofanyika Old Trafford. Wafungaji kwa upande wa Man United waliokuwa ni: Bryan Mbeumo aliifungia timu yake bao la kwanza na Bruno Fernandes akamalizia kwa bao la pili, akifanya magoli ya United kuwa 2–0. Ushindi huu unaifanya Manchester United kufikisha ushindi wa nne mfululizo katika Premier League, na kubaki nafasi ya 4 katika msimamo ikiwa na pointi 44. Katika mechi zijazo, United wataikaribisha West Ham United, wakati Tottenham Hotspur itacheza dhidi ya Newcastle United – michezo yote ikiendelea Februari 10, 2026.

Share this post: