Kwaresma 2026: Ratiba Rasmi ya Jumapili, Alhamisi Kuu na Pasaka… Ipo Hapa
2026-02-14 - 02:20
Safari ya Kwaresma ni kipindi cha toba, sala na tafakari kinachoandaa waumini kuadhimisha Ufufuko wa Kristo. Hiki ni kipindi muhimu sana ndani ya Roman Catholic Church na makanisa mengi ya Kikristo duniani. Hapa chini nimekuwekea ratiba kamili kwa mpangilio mzuri na rahisi kufuatilia Mwanzo wa Kwaresma Jumatano ya Majivu – Februari 18, 2026 (Mwanzo rasmi wa Kwaresma – ishara ya toba na unyenyekevu) Dominika za Kwaresma Dominika ya Kwanza – Februari 22, 2026 Dominika ya Pili – Machi 1, 2026 Dominika ya Tatu – Machi 8, 2026 Dominika ya Nne (Laetare – furaha katikati ya Kwaresma) – Machi 15, 2026 Dominika ya Tano – Machi 22, 2026 Wiki Kuu (Holy Week) Dominika ya Matawi – Machi 29, 2026 Alhamisi Kuu – Aprili 2, 2026 Ijumaa Kuu – Aprili 3, 2026 Jumamosi Kuu (Mkesha wa Pasaka) – Aprili 4, 2026 Jumapili ya Pasaka – Aprili 5, 2026