TheTanzaniaTime

Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei ameuawa, televisheni ya serikali Yathibitisha

2026-03-01 - 05:27

Taarifa kutoka Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran pamoja na vyombo kadhaa vya habari vya serikali vimethibitisha kifo cha Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, aliyekuwa na umri wa miaka 86. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Khamenei alifariki kufuatia mashambulizi ya pamoja yaliyoripotiwa kufanywa na Israel katika maeneo mbalimbali nchini Iran. Hata hivyo, maelezo rasmi kuhusu mazingira halisi ya kifo chake hayajawekwa wazi, wala haijatajwa wazi ni nani atakayechukua nafasi yake katika uongozi wa juu wa nchi hiyo. Kauli ya Rais wa Marekani Rais wa Marekani, Donald Trump, saa chache kabla ya uthibitisho huo, alieleza kuwa Kiongozi Mkuu huyo aliuawa katika operesheni maalum iliyolenga miundombinu muhimu ya Iran. Kauli hiyo imeongeza taharuki kimataifa, huku wachambuzi wa siasa wakitabiri mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati. Vyombo vya habari vya serikali pia vimeripoti kuwa baadhi ya wanafamilia wa Khamenei waliuawa katika mashambulizi hayo. Kwa mujibu wa Fars News Agency, shirika la habari linalohusishwa na Kikosi cha Revolutionary Guard, binti wa Khamenei, mkwe wake na mjukuu wake ni miongoni mwa waliopoteza maisha. Ripoti nyingine zinaeleza kuwa mmoja wa mabinti zake pia aliuawa, ingawa taarifa hizo bado hazijathibitishwa kwa kina.

Share this post: