TheTanzaniaTime

Kihongosi: TIA Kigoma Itakuwa Mkombozi wa Mkoa

2026-02-20 - 08:27

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi alisema ujenzi wa kampasi ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) mkoani Kigoma utakua mkombozi mkoani Kigoma kwa kutoa fursa kwa wanafunzi na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wakazi wanaozunguka maeneo ya chuo hicho. Kihongosi alieleza hayo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho uliofikia aailimia 95. Alisema CCM imeridhika na kazi iliyofanywa na serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia ujenzi wa chuo hicho ulioanza chinu ya uongozi wake June 2023. Ujenzi wa kampasi hiyo upo chini ya serikali kuu ukitegemea fedha kutoka Wizara ya Fedha na mpaka sasa zimetumika bilioni nane unatarajia kukamilika Machi 31, 2026 na kutoa fursa kwa wanafunzi wa mkoa wa Kigoma na nchi jirani ya Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kusoma katika kampasi hiyo.

Share this post: